In Samburu District, northern Kenya, men and women crafted collective belonging through and around colonial stereotypes of their ethnic sexuality. If administrators, missionaries, development workers, and journalists long invoked promiscuity and adultery to describe them as radical Others, rural Samburu turned to ritual to transform the implications of such stereotypes. In ceremonies called lopiro, they sought to end everyday adultery within particular generations and reimagine moral forms of collective belonging to age sets, clans, the state, and a world beyond Kenya. These ceremonies synthesized contradictions between the concrete socioeconomic and political struggles of rural Samburu families and the haunting colonial paradigms of their sexual alterity. Lopiro ceremonies demonstrate the central role of sexuality to autochthonous and ethnic forms of belonging in the postcolonial world. [sexuality, ethnicity, belonging, kinship, Samburu, Kenya]
Katika wilaya ya Samburu Kaskazini mwa Kenya, wanawake na wanaume wamejijengea utambulisho mpya wa jamii yao kupitia mgongo wa dhana potofu zilizozushwa na wakoloni juu ya mahusiano ya kimapenzi baina ya wanajamii wa jamii hiyo. Kwa muda mrefu, maafisa wa serikali, wamisionari, wafanyakazi katika miradi ya maendeleo, na waandishi wa habari wamekuwa wakitumia dhana ya “uzinzi” na “uasherati” wa watu wa Samburu kama kigezo cha kusisitiza tofauti kubwa ya kimaadili kati ya jamii ya Wasamburu na jamii zingine nchini Kenya. Kufuatia haya, Wasamburu walizigeukia mila zao na kuzitumia kama chombo cha ukombozi ili kuharamisha uzushi huo. Katika sherehe zao zinazoitwa lopiro, Wasamburu waliazimia kuharamisha na kufuta kila chembe ya uasherati iliyokuwemo miongoni mwa vizazi vyao na hivyo kudiriki kujitengenezea mfumo mpya wa maadili ya jamii nzima kwa ajili ya rika zote, koo zote, taifa la Kenya, na dunia nzima kwa ujumla. Sherehe hizi zilipelekea kuwepo na ukinzani mkali baina ya hali duni, iliyokithiri, ya kiuchumi, kijamii na kisiasa miongoni mwa familia za Samburu vijijini na jinamizi la dhana potofu za kikoloni juu ya mahusiano ya kimapenzi ya watu wa Samburu. Sherehe za lopiro zinaonesha kinagaubaga dhima ya mahusiano ya kimapenzi kama mhimili wa namna ambavyo jamii za kiasili zilivyojitambulisha na kuhusiana baada ya ukoloni. [mahusiano ya kijamii, kabila, udugu, Samburu, Kenya]
Im Samburu Gebiet im Norden Kenias stellten sich Männer und Frauen ihre kollektive Zugehörigkeit im Verhältnis zu kolonialen Klischees ihrer ethnischen Sexualität vor. Administratoren, Missionare, Entwicklungsarbeiter und Journalisten hatten die Samburu schon lange mit Promiskuität und außerehelichen Sex in Verbindung gebracht, um sie als kulturelle “Andere” zu beschreiben. Während der Kolonialherrschaft benutzten die Samburu Rituale, um die sozialen Folgen dieser Klishees abzuwandeln. In sogenannten “lopiro” Zeremonien versuchten die Samburu außerehelichen Sex zwischen bestimmten Generationen zu beenden und neue moralische Bezieungen zu Altersklassen, Clans, dem Staat and einer Welt jenseits von Kenia zu knüpfen. Diese Zeremonien stellten Widersprüche zwischen den konkreten sozioökonomischen und politischen Problemen der ländlichen Samburu Familien und einer kolonialen Weltanschauung ihrer sexuellen Alterität dar. Lopiro Zeremonien zeigen uns die wichtige Rolle der Sexualität im Bezug auf autochthone und ethnische Zugehörigkeit in der postkolonialen Welt. [Sexualität, Ethnizität, Zugehörigkeit, Verwandtschaft, Samburu, Kenia]
Figure 5. Over the microphone, the master of ceremonies praises the gifts exchanged on the last day of the lopiro ceremony. Samburu District, Kenya, December 2010.